Aisee DSTV!
SwahiliFix

Tanzania ‘mwendo mdundo’ kombe la dunia 2022 (+video)

Tanzania imefanikiwa kusonga mbele kwenye mechi za kufuzu kombe la Dunia 2022 nchini Qatar, Kwa kuitoa timu ya taifa ya Burundi kwa kuichakaza goli 3-0 kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

Taifa Stars ndio walikuwa wa kwanza kupata goli kipindi cha kwanza kupitia kwa Nahodha wake, Mbwana Samatta na baadae muda mfupi kabla ya mapumziko, Burundi wakachomoa goli hilo.

Kwenye hatua ya penati, Juma Kaseja amecheza penati mbili huku moja Warundi wakipiga nje ya goli.

Kwasasa hatua inayofuata Tanzania itaingia kwenye makundi ili kutafuta bingwa atakayefuzu kwenda Qatar kushiriki kombe la dunia mwaka 2022.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW