Habari

TANZIA: Viongozi wanne wa CUF wafariki kwa ajali wakitokea Dodoma

Viongozi wanne wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaomuunga mkono mwenyekiti wa chama hicho anayetambulika na Msajili wa Vyama, Prof. Ibrahim Lipumba wamefariki dunia usiku wa kuamkia Jumatano hii September 6, 2017, baada ya msafara wao kupata ajali maeneo ya Ubenazomozi Mkoa wa Pwani.

Gari ambalo linadaiwa kuhusishwa katika ajali hiyo.

Ajali hiyo mbaya imetokea wakati viongozi hao wakitokea Dodoma kwenye sherehe za kuapishwa kwa Wabunge wapya wa Chama hicho baada ya gari lao kugongana na Lori.

Akiongea na Bongo5 Jumatano hii, Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Abdallah Kambaya alisema viongozi waliofariki ni kutoka Wilaya ya Muheza, Tanga ambapo miongoni mwao ni Mgombea Udiwani wa Muheza Mjini, aliyefahmika kwa jina Uredi Ramadhani.

“Ni kweli kama mlivyosikia hiyo taarifa lakini mimi kwa sasa nipo Dodoma lakini viongozi wenzangu waliopo Dar es salaam wanaendelea kufuatilia hiyo suala na baada ya hapo nadhani watatoa taarifa rasmi ya nini kinaendelea,” alisema Kambaya.

Aidha, idadi ya majeruhi haijajulikana ila ni hawazidi 10 na baadhi yao wapo Hospital ya Tumbi huku akisema chanzo cha ajali hiyo ni gari la wafuasi hao kugongana na lori.

Bongo5 bado inaendelea kufanya mawasiliano na kamanda wa polisi mkoa wa Pwani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents