Habari

TCRA yajipanga kufunga simu zote zisizo na viwango vya ubora

Mamlaka ya mawasiliano nchini, TCRA inaandaa utaratibu wa kufunga simu zote ambazo hazina viwango vya ubora stahiki kwa lengo la kuzuia uingizwaji wa bidhaa hizo nchini ambazo zimekuwa zikiuzwa kiholela.

recycle_cell_phones

Meneja mawasiliano wa TCRA ‘Innocent Mungy’ amesema mamlaka hiyo kwa sasa inazunguka nchini kutoa elimu kwa wananchi ili wazitambue simu mbovu na madhara yake katika mawasiliano kabla ya kufikia zoezi hilo.

Zoezi litaanza kutoa tahadhari kwa wananchi kabla ya zoezi hilo ni kutokana na matokeo ya nchi ya Kenya ambayo ilitekeleza zoezi kama hilo Septemba mwaka jana, ambapo pamoja na malengo yao kutimia, wananchi wengi waliathirika pamoja na baadhi ya taasisi za serikali hasa sekta ya afya na biashara.

Ameongeza kuwa mwongozo wa kuzima simu wenye lengo la kukabiliana na uingizwaji wa simu bandia nchini, unatekelezwa kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2010 ya mawasiliano ya elektroniki na posta (EPOCA) pamoja na kanuni zake za mwaka 2011.

Source: Times Fm

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents