Habari

TCRA yampandisha kizimbani kinara wa kurudisha simu feki

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imemfikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Juma Maulidi, kwa kosa la kugushi simu feki zilizokwisha fungiwa na mamlaka hiyo na kuziwezesha kufanya mawasiliano kinyume na sheria ya mawasiliano.

Jambo hilo ni kinyume cha sheria kifungu namba 135 cha sheria namba 3 ya elekroniki na mawasiliano ya Posta ya mwaka 2010.

Akisoma mashtaka Hakimu Mkazi, Godyfrey Mwambapa na Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde wamesema mshtakiwa alitenda kosa hilo Novemba 8 mwaka 2016 katika eneo la Kariakoo mtaa wa Agrey jijini Dar es salaam, kwa kubadilisha namba ya utambulisho wa simu (IMEI) aina ya Tecno ambayo ilikuwa imefungiwa na TCRA.

Dhamana kwa mshtakiwa ilikuwa wazi ambapo walihitajika jumla ya wadhamini wawili kila mmoja akitakiwa kuwa na shilingi milioni 5 huku upelelezi wa shauri hilo umekamilika na mashtaka ya awali yamepanga kusomwa Mei 4 mwaka huu.

Kwa upande wake Mwanasheria Mwandamizi Mkuu wa TCRA, Johanes Kalungula, alizungumza na wanahabari nje ya Mahakama hiyo alisema jambo hilo linahatarisha usalama kwa watumiaji wa simu hizo.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents