Habari

TCRA yazitoza faini kampuni za simu

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imezitoza faini kampuni zote za simu kwa kusajili laini bila vitambulisho na kutofuata utaratibu za kusajili wa laini za simu.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba amesema kuwa kampuni hizo zimepigwa faini kutokana na kusajili laini mpya bila kutumia vitambulisho vinavyotakiwa.

Akizungumza leo katika Makao Makuu ya mamlaka hiyo amesema kuwa hiyo si mara ya kwanza kwa kampuni hizo kufanya kosa hilo, hivyo wameadhibiwa na faini ya ziada.

Kampuni ya Halotel imetozwa Shilingi milioni 822, Tigo Shilingi bilioni 625, Airtel Shilingi milioni 542, Vodacom Shilingi milioni 945, Zantel Shilingi milioni 52 milioni na Smart shilingi milioni 37.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents