AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Tetesi za Kayumba kutoka kimapenzi na Irene Uwoya ‘Ikitokea nafasi najitosa’

Muimbaji Kayumba ambaye ni zao la shindano la BSS, hivi karibuni amekuwa akihusishwa na kashfa nzito ya kutoka kimapenzi na aliyekuwa mke wa Dogo Janja, Irene Uwoya.

Tetesi hizo zilipamba moto mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka 2018 baada ya muimbaji huyo kum-wish birthday muigizaji huyo ujumbe ambao ulitafsiriwa za kiahaba.

Baada ya tetesi hizo kukuwa kila siku, Muimbaji huyo alibambwa na HZB alieleza kinaga ubaga mahusiano yake na mrembo huyo ambaye anatawa katika mitandao ya kijamii kutokana na mikato yake ya mavazi.

“Najisikia tu kiandika kuhusiana na Irene hata yeye huwa ananijibu,” alisema Kayumba.

Aliongeza, “Hata unapomuona anaimba nyimbo zangu anapenda muziki mzuri, kwahiyo amekutana na muziki nzuri kwangu. Kama zikitokea ishu za mahusiano hatuwezi kuzizuia,”

Mremboo huyo kutoka kiwanda cha filamu, amekuwa akihusishwa kuachana na rapa Dogo Janja lakini hakuna mmoja kati yao aliyewahi kuthibitisha hilo.

Hata hivyo mapema leo, Irene Uwoya alifunguka kuzungumzia skendo ya kuhusishwa anatoka kimapenzi wanaume mbalimbali.

“Mhhh wa bongo jamani loooh…mara natembea na Jon…mara Mussa…mara Jacob…mara nahis jirani…mara kasuku …mara urithiii …mara mafao ya Baba ake…mara hana lolote…dooohhh kweli kaz mnayo ndio maana hamna kaz zakufanya …jua likisogea na nyie mnasogea…daaah poleni sanaaa …kiufupi tu mnajisumbua …fanyeni maisha yenu kama mkishindwa njoooni insta mniview na kunilike pia kama huna bando semaaa tuuu nagawaga voucher na tena leo pia nitagawa nimekumbuka,Kaz ya mimi kuwa na nyumba au maendeleo niacheni mimi acheni kujipa majukumu yasiyowahusu…” aliandika Irene Uwoya.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW