Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya Ijumaa hii, Ramsey, Piatek, Sancho, Higuain, Origi na wengine sokoni

Aaron Ramsey ametia saini makubaliano ya awali ya mkataba wa kujiunga na Juventus kutoka Arsenal msimu huu.

Kiungo huyo wa miaka 28 tayari amekamilisha vipimo vya afya na mabingwa hao wa Italia wanaoshiriki ligi ya Serie A, wikendi iliyopita. (Sky Sports)

Ramsey anatarajiwa kutia saini mkataba wa miaka minne wa kitita cha euro milioni 300,000 kwa wiki, ambao utamfanya kuwa mchezaji wa Uingereza anaelipwa vizuri zaidi. (Times)

Chelsea wanajiandaa kumpatia Callum Hudson-Odoi, 18, dili mpya ambayo itagharimu kati ya euro 50,000 kwa wiki – hadi euro 70,000 – katika juhudi ya kumfanya asikubali ofa ya kujiunga na Bayern Munich. (Mail)

Juhudi za West Ham za kutaka kumnunua mshambuliaji wa Genoa na Poland Krzysztof Piatek, 23, zimegonga mwamba huku AC Milan wakijaribu bahati yao. (Mail)

Mkurugenzi wa soka wa klabu ya Borussia Dortmund Michael Zorci nayoshiriki ametoa wito kwa vilabu vya ligi kuu ya England dhidi ya uhamisho wa winga wa zamani wa Manchester City Jadon Sancho, 18. (Mirror)

Chelsea wanapania kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuain, 31, kutoka Juventus ili wamjumuishe katika kikosi kitakachomenyana na Arsenal Jumamosi hii. (London Evening Standard)

Chelsea pia wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa kati wa kimataifa wa Argentina Leandro Paredes, 24 anaechezea Zenit St Petersburg kwa kima cha euro milioni 31. (Express)

Manchester United wako tayari kuongeza malipo ya Marcus Rashford kwa hadi euro 150,000 kwa wiki ili kumzuia kiungo huyo wa miaka 21 asihamie vilabu vyovyote vikuu vya Ulaya msimu huu. (Mirror)

Tottenham wamefufufua azma yao ya kumnunua mshambuliaji wa Barcelona, Mbrazil Malcom, 21. (Independent)

Celtic wanafuatilia kwa karibu mchezo wa Scott McTominay wa Manchester United kwa lengo la kumnunua endapo kiungo wao wa kati ataondoka uwanja wa Parkhead. (Daily Record)

Liverpool wanamfuatili a kiungo wa kati wa Schalke Weston McKennie ,20. (Sun)

Meneja wa Arsenal Unai Emery amekiri kuwa wamefanya mazungumzo na Denis Suarez wa Barcelona lakini hakuna uwezekano wa kiungo huyo kusajiliwa mwezi huu. (Mirror)

West Brom wanapania kumsajili kwa mkopo mlinzi wa Bournemouth Tyrone Mings, 25. (Sun)

Meneja wa Everton Marco Silva amekiri kuwa wachezaji wengi wataondoka klabu hiyo kuliko wale watakaojiunga nao baada ya bodi ya usimamizi kusema hakuna fedha za kuwasaini wachezaji wapya. (Mail)

Meneja wa Fulham Claudio Ranieri ana mpango wa kumsaini kiungo wa kimataifa wa Burkina Faso Bryan Dabo, 26 anaechezea klabu ya Fiorentina. (Sun)

Mchezaji wa kwanza kusainiwa na klabu ya Manchester United katika msimu huu wa uhamisho wa wachezaji ni mshambuliaji wa Amiens ya Ufaransa Noam Emeran 16. (Manchester Evening News)

Inter Milan wakioo tayari kumpatia mkataba mpya mlinzi wa Slovakia Milan Skriniar, 23,ambaye pia ameusishwa na Manchester United na Manchester City. (Calciomercato)

Tottenham wanandaa mkutano wa dharura kujadili jinsi watakavyo kabiliana na ukosefu wa Kane uwanjani kwa miezi kadhaa.

Kuna uwezekano wakawasaini wachezaji wapya au kumpandisha cheo mshambuliaji Troy Parrott mwenye umri wa miaka 16. (Talksport)

Bayern Munich pia wanafanya mazungumzo ya kumsajili winga wa Chelsea Callum Hudson-Odoi. (Bild via Four Four Two)

Mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Ubelgiji Divock Origi, 23, ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na Tottenham baada ya Harry Kane, 25, kuumia. (Telegraph

Kipa wa Uhispania David de Gea, 28, anatarajiwa kutia saini mkataba mpya na Manchester United. (Mirror)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents