Aisee DSTV!
SwahiliFix

Tetesi za usajili, Makampuni ya kamari yameongeza dau juu ya uwezekano wa kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer kufutwa kazi

Tetesi za usajili, Makampuni ya kamari yameongeza dau juu ya uwezekano wa kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer kufutwa kazi

Makampuni ya kamari yameongeza dau juu ya uwezekano wa kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer kufutwa kazi baada ya kukubali kichapo cha kushtukiza dhidi ya Newcastle. Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino anapigiwa upatu kuchukua mikoba ya Solskjaer. (Sun)

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amedokeza kuwa mrithi wake klabuni hapo atakuwa kocha wa Rangers ya Uskochi Steven Gerrard ama kocha wa zamani wa klabu hiyo forme Kenny Dalglish.

Gerrard na Dalgish wote wameichezea Liverpool kwa mafanikio makubwa. (Star)

Beki wa zamani wa Liverpool Glen Johnson amemshauri mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 26, tkuihama klabu yake na kumpigia chapuo ajiunge na Man City. (Manchester Evening News)

Unai Emery

Kocha wa Arsenal Unai Emery anapiga hesabu za kumnunua beki wa Wolves Willy Boly. Wolves wanaweza kutaka dau la pauni milioni 20, wao walimnunua nyota huyo raia wa Ivory Coast kwa pauni milioni 10. (Sun).

Winga wa zamani wa Manchester United Ryan Giggs anaamini Ole Gunnar Solskjaer anatakiwa kusajili wachezaji wengine watano ili timu irejee kwenye kiwango chake. (Sun)

Real Madrid wapo tayari kuchuana na Juventus ikatika kinyang’anyiro cha kutaka kumsajili kiungo mkabaji wa Chelsea N’Golo Kante. Vigogo hao wa La Liga wanaweza kulipa dau la uasajili la kufikia pauni milioni 70 ili kumnasa Mfaransa huyo. (Sport, via Mail)

Ngolo kante

Kocha wa Bournemouth Eddie Howe amemtaka mshambuliaji wake Callum Wilson kuzipa kisogo tetesi kuwa Man United inataka kumsajili mwezi Januari. (Daily Echo)

Winga wa Chelsea Christian Pulisic,21, anaripotiwa kutaka kuomba kutolewa kwa mkopo kama hatapata muda mwingi zaidi wa kucheza klabuni hapo. (Sun)

AC Milan walikuwa kwenye mipango ya kutaka kumfuta kazi kocha Marco Giampaolo wakati wa mapumziko wa mechi dhidi ya Geonasiku ya Jumamosi. Mpaka mapumziko Genoa walikuwa wakiongoza kwa goli moja lakini mchezo uliisha kwa Milan kupata ushindi wa 2-1 (SempreMilan, via Star)

Christian PulisicHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Beki wa zamani wa pembeni wa Manchester United Alexander Buttner, 30, amesema alikataa maombi ya usajili kutoka klabu za Uskochi za Celtic na Rangers kabla ya kuamua kutimkia Marekani katika klabu ya New England Revolution. (Goal)

Mshambuliaji wa zamani wa Aston Villa Gabriel Agbonlahor, ambaye ndiye mshika rekodi ya kupachika mabao mengi zaidi kwa Villa amefichua kuwa wapinzani wao wa jadi klabu ya Birmingham City walijaribu kumsajili kutoka klabu ya Villa Park wakati alipokuwa mdogo. (Birmingham Live)

Nyota wa zamani wa Liverpool Steve McMahon amemdokeza kocha Jurgen Klopp kumsajili kiungo wa Leicester City James Maddison kabla ya wapinzani wao . (Stadium Astro, via Express).

TETESI ZA SOKA JUMAPILI

Ben ChilwellHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionLeicester City wanamsaka mchezaji atakayeichukua nafasi ya Ben Chilwell

Leicester City wanamsaka mchezaji atakayeichukua nafasi ya beki wa kushoto mwenye miaka 22 Ben Chilwell, huku Chelsea na Manchester City wakiongoza mvutano wa kumsajili mchezaji huyo wa timu ya taifa ya England. (Sun on Sunday)

Manchester United imekana kuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya taifa ya Ufaransa Paul Pogba anaomba £600,000 kwa wiki ili kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. Mkataba wa mchezaji huyo mwenye miaka 26 umesalia miaka miwili kabla ya kumalizika. (Sunday Mirror)

United wanataka kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth Callum Wilson ifikappo Januari na wanapanga kumvutia mchezjai huyo mwenye miaka 27 kwa kumpa nafasi ya kutimiza tuhuma zake za kufuzu katika klabu ya taifa ya England kwa michuano ya Euro 2020. (Sunday Express)

Arsenal itapambana na AC Milan katika kumsjaili mchezaji wa miaka 20 PSV Eindhoven Donyell Malen, na wapo tayari kutoa Euro 56m kwa raia huyo wa Uholanzi. (Tuttosport, kupitia Calciomercato)

Meneja wa Sheffield United Chris Wilder ana hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Brentford Ollie Watkins na atawasilisha obi la thamani ya £15m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Sun on Sunday)

United wanataka kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth Callum Wilson
Image captionMan United wanataka kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth Callum Wilson

Wakala wa mchezaji wa Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya Korea kusini Son Heung-min, mwenye miaka 27, amekataa kuondoa uwezekano wa kuwepo uhamisho katika siku zijazo wa mchezaji huyo kwenda katika timu ya Italia, Napoli(Calciomercato)

Mshambuliaji wa Red Bull Salzburg Erling Braut Haaland anasema uvumi unaomhusisha na uhamisho kwenda Arsenal na Manchester United ‘umechosha’. raia huyo mwenye umri w amiaka 19 kutoka Norway ameongeza kuwa anataka ‘kulindwa’ dhidi ya uvumi. (Football London)

Meneja wa Chelsea Frank Lampard amemuambia winga mwenye umri wa miaka 21 wa Marekani Christian Pulisic – aliyesajiliwa kwa £53m kutoka Borussia Dortmund – kuwa ada ya uhamisho wake haitoshi kupa nafasi ya kwenye kikosi cha kwanza katika timu hiyo (Sunday Mirror)

Frank LamaprdHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mlinzi wa Brazil David Luiz, mwenye umri wa miaka 32, anasema “hakufikiria mara mbili” kuhusu kujiunga na Arsenal kutoka Chelsea msimu wa joto, kwasababu alikuwa na fikra tofuati ya mchezo huo katika siku zijazo kwa Lampard. (Metro)

Aliyekuwa meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anafikiria kuhusu kuichukua nafasi ya kiufundi katika shirikisho la soka duniani Fifa, lakini raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wamiaka 68 haondoshi uwezekano wa yeye kurudi katika jukumu la usimamizi wa timu. (beIN Sports)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Newcastle United Sean Longstaff, mwenye umri wa miaka 21, ameambiwa asahahu ndoto yake ya uhamisho wa £40m kwenda Manchester United. (Sunday Mirror)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anasema shinikizo la kushinda mataji linafanya kuwa vigumu kuwachezesha wachezaji chipukizi kutoka chuo cha mafunzo cha klabu hiyo. (Sunday Telegraph)

Pep GuardiolaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPep Guardiola anasema shinikizo la kushinda mataji linafanya kuwa vigumu kuwachezesha wachezaji chipukizi Mancity

Aliyekuwa kapteni wa Arsenalna mlinzi Laurent Koscielny anasema aliiwacha Gunners akiwa anajivuni. raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 34 alijiunga na Bordeaux msimu wa joto.(Mail on Sunday)

Kipa wa Manchester United David de Gea ana hamu ya kuinunua klabu ya divisheni ya pili Uhispania Elche huku mchezaji huyo wa kimataifa mwenye umri wa miaka 28 akitakiwa kulipa £16m ili makubaliano hayo yafanikiwe. (Sport)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW