Habari

TFDA yakamata dawa bandia zenye thamani ya shilingi milioni 17.4

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekamata dawa bandia aina tano katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini. Miongoni mwa dawa hizo ni dawa za Malaria.

tfda-702x336

Akizungumza na waandishi wa habari Jumamosi hii, jijini Dar es salaam,Mkurugenzi mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo,amesema mamlaka hiyo ilifanya utafiti katika kanda hizo baada ya kupata taarifa za uwepo wa dawa bandia kwenye maeneo ya mikoa ya Geita na Mara katika kipindi cha mwezi Agosti na Septemba mwaka huu.

“Uchunguzi wa awali umeonesha kuwa dawa hizi bandia zinatengenezwa hapa nchini katika makazi ya watu na maeneo mengine ya kificho ambapo zilizoisha matumizi huongezewa muda kwa kuondolewa lebo za zamani na kuwekwa mpya,”amesema.

“Maduka 17 yaliyokutwa na dawa bandia na dawa za serikali yamefungwa, dawa zimekamatwa na pia inafungua majalada 38 katika vituo vya polisi dhidi ya watuhumiwa,” ameongeza.

Amesema TFDA imekamata dawa hizo bandia zenye thamani ya shilingi milioni 17.4 ambapo mkoa wa Mbeya umetajwa kuwa na idadi nyingi ya dawa hizo.

Aidha Sillo ametaja maeneo yaliyofanyiwa ukaguzi kuwa ni pamoja na famasi, maghala ya dawa, zahanati, maduka ya dawa za mifugo na muhimu na kwamba jumla ya maeneo 207 yalifanyiwa ukaguzi.

Mnamo Oktoba 4 hadi 6 2016 TFDA ilifanya operesheni maalumu ya ukaguzi kwa lengo la kubaini, kukamata, kuziondoa katika soko na kuwachukulia hatua za kisheria wanaojihusisha na biashara ya dawa bandia za serikali, zisizosajiliwa, pamoja na dawa duni na zile zilizoisha muda wake wa matumizi.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents