Habari

The New Yorker lamtaja Al-Shaymaa Kwegyir miongoni mwa waafrika 8 waliofanya makubwa – 2012

SAM_1250

Jarida la The New Yorker limemtaja Al-Shaymaa Kwegyiris miongoni mwa waafrika wanane waliofanya mambo makubwa zaidi kwa mwaka 2012 katika makala yake ya ‘The Eight Most Fascinating Africans of 2012’.

Akiwa mbunge, Kwegyiris aliekeleza jitihada zake nyingi katika kutetea haki za maalbino nchini waliokuwa wakiuawa kikatili kutokana na imani za kishirikina.

Wengine waliotajwa kwenye orodha hiyo ni pamoja rais wa Malawi Joyce Banda, mwanasheria wa Cameroon Alice Nkom, director wa filamu ya “Nairobi Half Life,” David (Tosh) Gitonga na mbunge mwenye umri mdogo zaidi barani Africa kutoka Uganda.

Wengine ni mwandishi wa habari wa nchini Afrika Kusini Justice Malala, wasanii wa kundi la P-Square wa Nigeria na rais wa Rwanda Paul Kagame.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents