Burudani

Thuto ya Cassper Nyovest yazipiku albamu za mastaa duniani

Rapper kutoka nchini Afrika Kusini, Refiloe Maele Phoolo maarufu kama Cassper Nyovest anazidi kusherekea mafanikio yake kwenye muziki.

Albamu yake mpya ‘Thuto’ ambayo iliachiwa mwezi Mei 7 mwaka huu ikiwa na nyimbo 16 imefanikiwa kushika namba moja katika mwezi mei katika soko la mauzo ya albamu huko Afrika Kusini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Cassper ameonyesha kufurahia hatua hiyo aliyoipiga kwa kuandika, “Number 1 album for 1 month straight!!! Thank you for the support !!! Click on the Link in my bio to buy/stream #Thuto.” Album hiyo imeshirikishwa wasanii kibao wakiwemo Goapele, Tshego, Tsepo Tshola, Nadia Nakai na Black Thought.

‘Thuto’ imefanikiwa kuzipiku albamu nyingine za mastaa wakubwa kama ‘Damn’ ya Kendrick Lamar, ‘Curtain Call’ ya Eminem, ‘More Life’ ya Drake, ‘Future’ ya rapper Future na nyingine.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents