Michezo

Torres atimiza ndoto yake baada Atletico Madrid kutwaa ubingwa wa Europa League

Mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid, Fernando Torres ameelezea furaha yake baada ya klabu yake kutwaa ubingwa wa Europa League mwaka 2017/18.

Torres amesema kuwa ametimiza lengo lake akiwa na Atletico Madrid na hiyo ndiyo ilikuwa ndoto yake kubwa kutwaa kombe kubwa la Ulaya akiwa na timu yake ya utotoni Atletico Madrid.

Kusema ukweli hili ndilo taji kubwa ambalo sijawahi kushinda tangu niwe na klabu yangu pendwa, hii ni furaha kwa timu na mashabiki wetu lakini kwangu ni zawadi tosha,“amesema Torres kwenye mazungumzo yake na waandishi wa habari baada ya kumalizika mchezo huo wa fainali jana usiku.

Mkongwe Torres amecheza mechi 403 akiwa na Atletico Madrid lakini hajawahi kutwaa taji kubwa barani Ulaya katika awamu zote alizoitumikia klabu hiyo.

Jana usiku klabu ya Atletico Madrid imetwaa ubingwa wa kombe la Europa League kwa kuichakaza klabu ya Marseille goli 3-0 kwenye mchezo wa fainali uliopigwa kunako dimba la Groupama.

Magoli ya Atletico Madrid yamefungwa na Antoine Griezmann x2 na moja likifungwa na Gabi.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents