Habari

Uchaguzi Zambia: Rais Edgar Lungu aibuka mshindi

Rais wa Zambia Edgar Lungu ametangazwa mshindi matokeo ya uchaguzi wa urais kulingana na matokeo rasmi ya uchaguzi huo.

du

August 15 2016 Tume ya uchaguzi nchini Zambia ilimtangaza aliyekuwa rais wa Zambia, Edgar Lungu kuwa ndo mshindi wa nafasi hiyo ya urais kwa tiketi ya chama cha Patriotic Front kwa awamu ya pili. Lungu alipata asilimia 50.35 ambazo ni sawa na kura 1, 860, 877 na Kumshinda mpinzani wake Hakande Hichilema wa chama cha United Party for National Development ambaye amepata asilimia 47.67 ambazo ni kura 1, 760, 347.

Matokeo hayo yametangazwa Jumatatu hii japo mpinzani wake, Hakainde Hichilema akidai kuna udanganyifu katika uhesabuji wa kura. Matokeo hayo yamempa ushindi Rais Lungu kwa zaidi ya kura laki moja mbele ya mpinzani wake huyo wa karibu.

Siku ya Jumapili, Hichilema akiongozana na wafuasi wake, walifika kwenye makao makuu ya tume ya uchaguzi ya Zambia ambako matokeo yanatangaziwa akitaka kukutana na mwenyekiti wa tume, lakini hata hivyo alizuiliwa na Polisi.

Hichilema wa UPND ameyapingwa matokeo hayo.

Anadai kulikuwa na udanganyifu mkubwa wa kura kwenye jimbo la Lusaka na maeneo mengine ya nchi, ambako anasema tume ya uchaguzi ilichelewa kutangaza matokeo yake kwakuwa yalikuwa yakitengenezwa ili kumpa ushindi Rais Lungu ambaye anatetea kwa mara nyingine nafasi yake.

Uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa wa upinzani mkali kati ya Rais Lungu, ambaye pia alimshinda Hichilema kwenye uchaguzi uliopita kwa kura elfu 28, na safari hii mchuano ulikuwa mkali zaidi kutokana na upinzani ulioshuhudiwa.

Hata hivyo wadadisi wa mambo wanaamini kuwa uchaguzi wenyewe ulikuwa na mapungufu, ikiwemo vitisho kwa baadhi ya maofisa wa tume, lakini kwa sehemu kubwa wanakubaliana kuwa ulifanyika kwa huru na haki.

Waangalizi wengi wa kimataifa kwenye ripoti zao za awali waliwapongeza wananchi wa Zambia kwa kushiriki uchaguzi kwa amani licha ya dosari ndogondogo ambazo walizibaini ingawa hawajasema ikiwa uchaguzi ulikuwa wakuaminika.

Wakati akihitimisha kampeni zake Rais Lungu aliahidi kuilinda katiba ya nchi kwa kuhakikisha usalama wa raia dhidi ya watu waliodaiwa kutaka kufanya vurugu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents