Habari

Tumkumbuke Lissu katika sala majira ya kujaribiwa kwake – Mhe. Nyalandu

Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Mhe Lazaro Nyalandu amewaomba wana Singida na Watanzania wote waendelee kuchangia gharama za matibabu ya Mhe. Tundu Lissu huku akiomba akumbukwe mbunge huyo katika sala na dua.

Nyalandu kupitia ukurasa wake wa instagram kuwa akumbukwe katika majira na saa hii ya kujaribiwa kwake.

TUNAWAOMBA WANA Singida na WATANZANIA WOTE tuendelee kuchangia gharama za MATIBABU ya Mh.Tundu Lissu. SOTE tumkumbuke katika SALA na DUA zetu katika majira na saa hii ya kujaribiwa kwake. MUNGU akisema NDIO, hakuna awezaye KUPINGA. KWA wote wanaohusika moja kwa moja kumtibu na kumtunza, MIKONO yao na FAHAMU zao zikahuishwe katika UBORA wote wa utabibu na matunzo. MAZUNGUMZO yanayoendelea na MADAKTARI BINGWA na hospitali mahiri kote duniani yafanikiwe upesi kumwezesha Mh. Lissu kuifikia huduma bora ya matibbu iliyopo kwa SASA ulimwenguni. IWE HERI KWAKE. #MUNGUIBARIKITANZANIA #NAWATUWAKE #PRAYFORTUNDULISSU

Lissu alijeruhiwa kwa kupigwa risasi Septemba 7 mwaka huu, mjini Dodoma eneo la ‘area D’ na watu wasiojulikana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents