Burudani

Tundaman apanga kumshirikisha Fally Ipupa kwenye wimbo wake ‘Hasara Roho’

Hitmaker wa Msambinungwa Tunda Man amedai kuwa anatarajia kumshirikisha nyota wa miondoko ya dance kutoka DRC, Fally Ipupa katika ngoma yake mpya ya Hasara Roho.

Tundamani

“Kuna ngoma inaitwa Hasara Roho nataka kumshirikisha Fally Ipupa, kwahiyo nasikilizia mpango huo nimeshamtumia beat na vocal kwahiyo nasubiri na yeye anitumie,” Alifunguka msanii huyo kupitia kipengele cha Chumba Cha cha Bomba Base Show ya Bomba FM Radio ya Mbeya.

Katika hatua nyingine Tunda alielezea sababu ya kumshirikisha Ally Kiba kwenye wimbo wake Msambinungwa: Ally Kiba ni mtu fulani ambaye kiukweli nilikuwa namtamani kufanya naye ngoma muda mrefu sema nilikuwa sijapata ngoma ambayo atafiti vizuri, isitoshe amekaa kimya muda mrefu, kiukweli ile ngoma ameiimba kitofauti sana Ally Kiba alinipa Chalenge sana.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents