Habari

Tungepambana na Kubenea, Sumaye, Lowassa ningewatoa ulingoni – Profesa Lipumba

Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba amesema kitendo cha yeye kunyamaza wakati umoja wa Katiba UKAWA  walivyoanzisha kampeni yao ya ondoa msaliti Buguruni alitumia busara tu kwani angetumia nguvu wahusika wote wa walioanzisha kampeni hiyo angewatwanga masumbwi mara moja licha ya uzee alionao.

Tokeo la picha la lipumba
Mhe Lowassa kushoto akisalimiana na Profesa Lipumba

Akiongea mbele ya waandishi wa habari leo makao makuu ya Chama cha Wananchi (CUF) Buguruni jijini Dar es salaam, Lipumba amesema alikuwa na uwezo wa kuwagaragaza ulingoni kama angeamua kutumia nguvu lakini alitumia busara kwa kufuata taratibu kuweza kupata suluhisho la mbasuko uliokuwa unaletwa ndani ya CUF na CHADEMA.

“Katika inasema msemaji mkuu wa mambo ya CUF  ni Mwenyekiti mkuu wa CUF taifa, Hao (CHADEMA) wakajenga mazingira kuwa Freeman Mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA kuwa msemaji wa Chama cha CUF, halafu wanadiliki kwenda kukaa na Wabunge wa CHADEMA….na Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya pwani anasema ametumwa na Mhe Lowassa kuandaa operation ya ONDOA MSALITI BUGURUNI…. muda huo huo wabunge wa CUF wapo”,amesema Lipumba wakati akifafanua sababu za kuwavua uanachama wabunge nane huku akijigamba kuwa ametumia taratibu tu kwani angetumia nguvu angewachakaza ulingoni.

“Kubenea namfahamu siku nyingi pamoja na uzee wangu huu ningeweza kusema Kubenea wakuweza kumshughulikia mimi mara moja, lakini hapana tunafuata taratibu za kisheria ningeweza kueleza yeye mwenyewe amchukue na Mwenyekiti wake wa kanda Sumaye, amtafute na Lowassa wamuite na Maalim Seif awe refarii halafu tuingie kwenye dimba tuweze kupambana nao ningeweza kuwaondoa wote na nikamshughulikia na refa wao.. ndiyo maana baada ya kuanzisha ile operation ya ONDOA MSALITI BUGURUNI na kutoa vitisho nikaamua kuchukua hatua za kuchukua taratibu”,amesema Profesa Lipumba.

NEC yateua Wabunge 8 wa Viti Maalum CUF

Hata hivyo Profesa Lipumba amelishukuru bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Spika wa Bunge, Job Ndugai kwa kukubali ombi loa la kuwafuta ubunge, wabunge nane wa CUF waliofutwa uanachama kwa makosa ya kukisaliti chama.

By Godfrey Mgallah

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents