Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

TV1 kuonyesha Ligi Kuu ya England

Mashabiki wa soka nchini wamepata ahueni ya kutazama Ligi Kuu ya England kupitia kituo cha runinga cha TV1.
mEJA
Meneja wa TV1, Joseph Sayi

Meneja Mkuu wa TV1, Joseph Sayi amesema kituo chao kimepata ruhusa kutoka kampuni ya Econet Media yenye haki za kuonyesha ligi hiyo kusini mwa Jangwa la Sahara.

“Kama inavyofahamika kuwa Ligi Kuu England inatazamwa na watu zaidi ya milioni 260 duniani, hivyo tumeona tuwafikishie uhondo huu mashabiki wa soka nchini kwa urahisi,” amesema Sayi.

Meneja Masoko wa TV1, Gillian Lugumamu amesema kituo hicho kitaonyesha mechi moja kila Jumamosi, huku Ijumaa na Jumatano zikitengwa kwa ajili ya uchambuzi wa mechi za ligi hiyo.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW