Michezo

TWFA yatangaza ratiba ya uchaguzi mkuu  

 

Chama cha Mpira wa Miguu wanawake (TWFA), kimetangaza rasmi tarehe ya uchaguzi mkuu ambao utafanyika Julai 8 mwaka huu.

Wakwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Miguu Wanawake (TWFA)  Amina Karuma akifafanua jambo

 

Chama cha Mpira wa Miguu wanawake (TWFA), kimetangaza rasmi tarehe ya uchaguzi mkuu ambao utafanyika Julai 8 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa (TWFA), George Mushumba amesema kuwa fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho zitaanza kutolewa Juni 19 huku mwisho wa kurudisha fomu hizo ikiwa ni Juni 22.

Kamati hiyo imetoa ratiba ya kuelekea uchaguzi huo ambapo Juni 23 mwaka huu kamati ya uchaguzi itapitia majina ya wagombea walioomba nafasi mbalimbali.

Juni 24 kamati ya uchaguzi itatangaza majina ya wagombea waliostahili au waliotimiza taratibu za uchaguzi kwa mujibu wa katiba au kanuni za TWFA.

Pingamizi ya uchaguzi huo yatapokelewa kati ya Juni 26 na 27 mida ya saa 4:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni na pingamizi yote kupitiwa  Juni 28.

Juni 29 kamati hiyo itatoa majumuisho ya pingamizi huku  tarehe 30 wagombea wote kufanyiwa usaili kabla ya mwezi Julai kutangaza majina ya wagombea waliopitishwa

Kamati hiyo iliyo chini ya mwenye kiti huyo inatarajia kupokea rufaa Julai 02, huku nafasi zitakazo gombewa katika uchaguzi huo ni pamoja na nafasi ya Mwenyekiti, Makamu mwenyekiti, Katibu mkuu, Katibu msaidizi, Mweka hazina, Mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF pamoja na wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji.

BY HAMZA FUMO

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents