Michezo

Ubaaguzi wa rangi unavyoendelea kukithiri kwenye soka, Shabiki akamatwa kwa kumpiga kichwani mchezaji wa Man United – Video

Ubaaguzi wa rangi unavyoendelea kukithiri kwenye soka, Shabiki akamatwa kwa kumpiga kichwani mchezaji wa Manchester United - Video

Mwanamume mmoja amekamatwa baada ya kuoneka kufanya isahara za kima au tumbili kwa wachezaji wa Manchester United wakati wa mchuano wa Jumamosi hii. Polisi wanasema walipokea taarifa kwamba shabiki mmoja anafanya ishara zinazominika kuakisi ubaguzi wa rangi wakati wa mechi dhidi ya Manchester City.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 41, anashikiliwa kwa madai ya kuchochea umma.

Wasimamizi wa FA wanapanga kuzungumza na refa wa klabu hiyo Anthony Taylor na polisi.

Tukio hilo lilitokea pale kiungo wa kati Fred alipokuwa amekwenda kupiga mpira wa kona katika kipindi cha pili na akapigwa na kitu kilichotoka kwa mashabiki.

Baada ya mechi, Fred alisema: “Nikiwa uwanjani sikuona chochote. Nilikiona baadaye katika chumba cha kubadilisha nguo. Watu walinionesha aliyekirusha kitu hicho ambacho kilinipiga.”

Tabia isiyokubalika

Kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer amesema: “Fred na Jesse walikuwa kwenye kona, na nimeiona video hiyo na pia kuzungumza na vijana wangu.”

Solskjaer ameongeza kuwa tabia hiyo iliyonakiliwa kwenye kamera ni jambo lisilokubalika.

Wakufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer na mwenzake City Pep Guardiola wamelaani vikali tukio hilo
Wakufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer na mwenzake City Pep Guardiola wamelaani vikali tukio hilo

Katika taarifa, Manchester City imesema inashirikiana na polisi kutambua wahusika pamoja na kuchunguza suala la kutupa kitu uwanjani.

“Klabu hii haivumilii vitendo vyovyote vya ubaguzi wa rangi na yeyote atakayepatika na hatia atapigwa marufuku na klabu hii milele.”

Supt Chris Hill amesema: “Ni matumaini yangu kwamba kukatwa kwa mtu huyu kunaonesha kwamba jambo hili tunalichukulia kwa uzito mkubwa.

“Tutaendelea kushirikiana na vlabu vya Manchester City na Manchester United nna pia tutaendelea kufanya uchunguzi wa aina yoyote ile utakaohitajika.”

Hili linatukia mwaka mmoja baada ya suala la ubaguzi wa rangi kugonga vichwa vya habari.

Fred baadae aliungana na wachezaji wenzake wa United kusherehekea ushindi wao wa mabao 2-1dhidi ya City katika uwanja wa EtihadFred baadae aliungana na wachezaji wenzake wa United kusherehekea ushindi wao wa mabao 2-1dhidi ya City katika uwanja wa Etihad

Kisa hicho kinajiri mwaka mmoja baada ya suala la ubaguzi wa rangi katika soka kugonga vichwa vya habari pale mshambuliaji wa City Raheem Sterling, alipotukanwa kwa mishingi ya rangi yake ya ngozi yake katika uwanja wa Stamford Bridge, hali illiyosababisha shabiki wa Chelsea kupigwa marufuku ya daima.

Sterling ni miongoni mwa wachezaji wa England waliofananishwa na tumbili na kupewa salamu za Wanazi katika mechi za kufuzu kwa kombe la Euro 2020 mwaka huu. Fred amesema tukio la Jumamosi ”linaonesha jinsi ambavyo tumejikita katika mambo ya kitambo yasiyokuwa na tija.”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents