Habari

Uchaguzi wa Nigeria wasogezwa mbele kwa wiki moja

Uchaguzi wa urais na ubunge nchini Nigeria umesukumwa mbele kwa wiki moja.

Tume huru ya kitaifa ya uchaguzi (INEC) ilitangaza hatua hiyo saa tano tu kabla ya wapiga kura kuelekea katika vituo vya upigaji kura hii leo Jumamosi.

“Haiwezekani kuendelea na zoezi la uchaguzi kama ilivyopangwa,” mwenyekiti wa tume hiyo Mahmood Yakubu amesema, akitaja hitilafu za kimipango.

Amesema uamuzi huo mgumu umehitajika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa huru na haki.

Uchaguzi wa urais na ubunge umepangiwa sasa kufanyika Jumamosi ijayo Februari 23.

Uchaguzi wa Ugavana, wawakilishi wa majimbo na mabaraza ya manispaa yamepangiwa kufanyika Jumamosi Machi 9.

Uamuzi huo umetolewa baada ya mkutano wa dharura katika makao makuu ya tume hiyo ya uchaguzi katika mji mkuu Abuja.

Bwana Yakubu amesema uamuzi huo umechukuliwa baada ya ‘ukaguzi wa makini’ wa ‘mpango ya namna uchaguzi utakavyofanyika’, akiongeza kwamba kuna ‘jitihada kubwa za kuhakikisha kuna uchaguzi wa huru, haki na wa kuaminika’.

Amesema ni muhimu kuchelewesha uchaguzi huo kuipa tume nafasi ya kukabiliana na masuala muhimu na pia “kusalia na hadhi katika uchaguzi”, lakini hakutoa ufafanuzi zaidi.

Source: BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents