Michezo

UEFAChampionsLeague: Real Madrid waendeleza ubabe Ulaya (+Video)

Mabingwa watetezi wa kombe la Klabu bingwa barani Ulaya, Real Madrid usiku wa kuamkia leo wameendeleza ubabe kwa kuichakaza klabu ya APOEL Nicosia, goli 3-0.

https://youtu.be/3fE2CO3biWU

Magoli ya Real Madrid yamefungwa na sio mwingine, Mreno Cristiano Ronaldo ambaye alitupia magoli mawili kabla ya beki mtata, Sergio Ramos akipigilia msumali wa mwisho kunako dakika ya 61 kipindi cha pili.

Kwa matokeo hayo Madrid wanaongoza kundi H, huku Tottenham Hotspur wakiwa nafasi ya pili baada ya jana kuitwanga Borrusia Dortmund goli 3-1.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents