Habari

UGANDA: Mwanafunzi wa miaka 10 amuua mwenzake wa miaka 16 kisa wivu wa mapenzi na kutoroka na baba yake

UGANDA: Mwanafunzi wa miaka 10 amuua mwenzake wa miaka 16 kisa wivu wa mapenzi na kutoroka na baba yake

Polisi wilayani Bududa Mashariki nchini Uganda wanamsaka mwanafunzi wa miaka 10 katika shule ya msingi Buwali aliyetoroka na baba yake mara baada ya kumchoma kisu na kumuua mwenzake kwa kisa kilichodaiwa kuwa aliporwa mpenzi wake.

Polisi walimtambulisha mwathirika au mwananfunzi aliyechomwa kisu akijulikana  Sam Watsosi miaka 16. Watsosi alidaiwa kuchomwa kisu siku ya Jumapili kwa tuhuma kwamba alikuwa akitembea au kuwa na mahusiano ya kimapenzi na kijana ambaye alikuwa mpenzi wa mwanazi aliyefanya tukio hilo.
Baada ya tukio hilo, lililotokea katika kituo cha biashara cha Bunamubi Kata ya Bukigai Sub, Watsosi alikimbizwa katika hospitali ya Bududa akitokwa na damu nyingi.
Na kuelezwa siku inayofuata yaani Jumatatu jioni Watsosi alipoteza maisha, Watsosi imeelezwa kuwa alikuwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Bulucheke wilayani Bududa.

Baada ya tukio hili Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Bududa (DPC) Bwana Jaffar Magayisi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la mauaji na wamesema.

“Tunamsaka mwanafunzi huyo, ambaye kwa sasa amekimbia na baba yake kufuatia kifo cha mwenzake,”

Tukio hilo limetokea siku ya Jumapili ambapo baada ya kutokea kwa tukio hilo Watsosi alikimbizwa hospitali ya Bududa akiwa anavuja damu nyingi hali iliyopelekea kupoteza maisha siku ya jumatatu jioni.

Kuna mvutano mkubwa katika eneo hilo kwani ndugu za marehemu walitishia kushambulia familia ya mtuhumiwa kwa kulipiza kisasi.

Kwa mujibvu wa Daily Monitor DPC aliwataka familia ya Watsosi itulie, akisema mtuhumiwa atakamatwa na kushtakiwa kwa mauaji mahakamani.

Bwana Charles Mutabali Kibeti, mwenyekiti wa LCIII amesema “Inashangaza sana kuwa mtoto wa miaka 10 anaweza kuwa na rafiki wa kike, ambaye yuko tayari kufanya chochote kumlinda akiwa na umri mdogo,”

 

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents