Marekani yatekeleza adhabu ya kifo kwa mtu mmoja ambaye alikutwa na hatia ya kumuua mkewe miaka 15 iliyopita

Texas imetekeleza hukumu ya kwanza ya kifo kwa mwaka 2020 nchini Marekani, kwa kumuua kwa sindano ya sumu mtu aliyekutwa na hatia ya kumuua mkewe miaka 15 iliyopita kwa sababu alidai talaka.

John Gardner (64), alihukumiwa kifo mnamo 2006 kwa kumuua mkewe wa tano, adhabu ambayo imetekeleza tarehe 15 januari 2020.

Gardner alivunja nyumba mpya ya Tammy Gardner (Mkewe) na kumpiga risasi kichwani wiki mbili kabla ya talaka kukamilishwa.

Waendesha mashtaka wanasema Gardner alikuwa na historia ya muda mrefu ya dhuluma dhidi ya wake zake. Alimpiga risasi mkewe wa pili alipokuwa mjamzito.

Alikuwa pia amemteka nyara mke wake wa tatu na kumpiga binti yake, waendesha mashtaka wanasema.

Related Articles

Back to top button