Habari

Ugonjwa wa Ebola yatinga DRC

By  | 

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa ugonjwa wa Ebola umezuka katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Eugene Kabambie ni msemaji wa WHO nchini humo amesema kuwa shirika hilo limeanza kuchukua hatua baada ya watu watatu kufariki wakihisiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola. Pia WHO imesema mlipuko huo unaathiri maeneo ya msituni ya Aketi, katika mkoa wa Bas-Uele karibu na mpaka wa nchi hiyo na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Waziri wa Afya wa DR Congo, Oly Kalenga kupitia barua, amesema kuwa watu tisa kutoka eneo la kiafya la Likati, Aketi waliohofiwa kuwa na Ebola.Watano kati yao walipimwa na mmoja wao akathibitishwa kuwa na virusi hivyo na watatu walifariki.

Mwaka 2014, mkurupuko wa ugonjwa wa Ebola katika Jamuhuri ya demokrasia ya Congo ulidhibitiwa kwa haraka ingawa watu 49 walifariki. Na watu waptao watu zaidi ya 11,000 walifariki kutokana na mkurupuko wa Ebola Afrika Magharibi 2014-2015, sana nchini Guinea, Sierra Leone na Liberia katika mlipuko wa Ebola ulioatajwa kuwa mbaya zaidi kuwahi kutokea duniani.

Mlipuko huo wa sasa ni wa nane kutokea nchini DR Congo tangu mwaka 1976.

Na Laila Sued

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments