Soka saa 24!

Uhuru Kenyatta kuapishwa April 9 kama Rais wa 4 wa Kenya

Rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta na makamu wake William Ruto wataapishwa rasmi April 9 baada ya mahakama kuu leo kuhalalisha ushindi wake.

Uhuru_M_Kenyatta_685841119

Waziri mkuu Raila Odinga aliwasilisha malalamiko katika mahakama hiyo kuwa uchaguzi haukuwa wa haki.

Jaji mkuu wa mahakama kuu ya Kenya Dr Willy Mutunga amesema kuwa benchi la majaji sita limethibitisha kuwa uchaguzi ulifanyika kwa uhuru, haki na wazi na kwa kuzingatia sheria za nchi.

Majaji wamekubaliana pia kuwa Uhuru Kenyatta na William Ruto walichaguliwa kihalali.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW