Burudani

Ulinzi waongezwa kwa Ariana

Baada ya shambulio la kigaidi jijini Manchester Uingereza, msanii Ariana Grande na amua kutimkia Boca Ration kwa mama yake, hali ya ulinzi imezidi kuimarishwa.

Ariana aliyetangaza kurudi jijini Mancherster kutoa pole kwa mashabiki wake Juni 5, huwenda hatua hiyo ikachukua muda baada familia yake kumuongezea ulinzi kwa kumuwekea mlinzi binafsi mmoja na walinzi wawili wa kujitegemea.

Mama yake na Ariana, Joan ameamua kumpa mlizi wa ziada binti yake awapo mjini,pamoja na uwepo wa polisi lakini familia hiyo inahofia juu ya usalama wa binti yao, kimeeleza chanzo cha karibu.

Wiki iliyopita katika tamasha “Dangerous Woman” la msanii huyo kulitokea mlipuko wa shambulio la kigaidi na watu wapatao 22 walifariki na wengine 59 kujeruhiwa kutokana na mlipoko huyo uliotokea katika ukumbi wa Mancherster Arena.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents