Habari

Una furaha? Usiipoteze kwa kufanya vitu hivi

Watu wengine wanapenda kuwa ovyo ovyo. Kama ungeweka kuwa na muda wa kutosha na fedha ungeweza kuwa na furaha tele. Lakini hicho hakiwezi kutokea kamwe. Furaha imewekwa kwa watu fulani tu, si kila siku mtu atakupenda na afanye ufurahi. Cha kushangaza kila mtu anasema anataka kuwa na furaha lakini hakuna anayejua furaha ni nini maishani?

happy-lady

Furaha ya maisha imetafsiriwa tofauti na walimwengu wakatudanganya. Sijaribu kupunguza uzito wa jambo lolote lile bali tuliambiwa furaha ni pale utakapokuwa kwenye nyumba nzuri na kubwa, ukiwa na gari na mambo mengine mengi. Swali la kujiuliza wangapi wana furaha mpaka hapo?  Furaha si kufanya vitu vingi ila ni kufanya vichache na kupata kuridhika ndani yako, lazima uondoe vitu ambavyo si vya muhimu kwenye maisha yako.

Ukweli ni kwamba si kitu wanachofanya watu wenye furaha kinawafanya wa tofauti ila ni namna wanavyochagua cha kufanya na cha kutokufanya huo ndio utofauti wao na sisi ambao tunatafuta furaha sehemu tofauti kabisa.

Wao huepuka sana mazingira hasi, tabia mbaya na maisha ya kimaskini. Watu wenye furaha huruhusu hali ya furaha kwenye maisha yao. Mwisho wa kusoma makala hii utagundua vitu vingi vinavyokufanya usiwe na furaha na jinsi gani ya kuviondoa ili uwe na furaha. Kuwa na furaha si ngumu kama unavyofikiria;

1. Watu wenye sumu

Inawezekana umewahi kusikia sheria namba tano ambayo inasema ‘watu watano ambao unatumia muda nao wanaathiri kwa kiasi kikubwa mwonekano wako wewe binafsi’. Hivyo unapopoteza muda na watu wenye mawazo hasi, akili mgando utatumia nguvu nyingi sana kuwa na furaha kwenye maisha yako.  Inahitaji ujasiri kuwaepuka watu wa jinsi hiyo ili upate furaha yako unayohitaji.

2. Kukimbizana kwa kuchelewa

Kulala sana na ukapitiliza inakufanya kwanza siku na hali mbaya au mtazamo ambao si sahihi. Utaanza siku kwa kukimbizana na kila kitu na mwisho wa siku unajikuta kama mambo hayaendi vizuri unapata mawazo mengi. Kuna wakati inakuwa ngumu kukwepa hili bali unapolifanya mara nyingi, uwezekana wa kuwa na furaha ni mdogo kwa kuwa unakuwa unakimbizwa na muda wakati wote. Jifunze kujipanga na kwanza vitu mapema ili uvimalize mapema.

3. Ulevi usiokuwa na tija

Uvutaji na unywaji mara zote unakuja akilini na hata tabia ya siku haipiti bila kunywa au kuangalia runinga masaa 3 usiku vinaathiri furaha yako. Haimaanishi televisheni ni mbaya au kuangalia mpira usiku wa manane ni vibaya, kitu cha kuangalia hapo je ni kujiuliza umekuwa mlevi wa vitu fulani? Hebu jaribu mwishoni mwa wiki kuachana na baadhi ya tabia ulizonazo, je utakuwa na muda gani huru ukiamua kutoangalia runinga kwa masaa matatu?

4. Kutindikiwa na vyombo vya habari

Watu wengi huachana na vyombo vya habari na habari zenyewe kujaribu kuondokana na mambo hasi kwenye maisha yao. Wanaamini kama kuna kitu wanatakiwa kujijua watasikia watu wakiongelea na habari zitawafikia tu. Na mpango huu unawasaidia sana watu wengi, ingawa kuna watu wanatamani kujua kila kitu kinachoendelea duniani. Jawabu la tatizo lake ni kwamba, tuna habari nyingine kwamba utaangalia ukiwa nyumbani au mchana wakati wa kupumzika huhitaji kuendelea kufuatilia mambo kana kwamba unalipwa kwa kusoma kila kitu, uwe unachagua vitu vya kusikiliza au kufuatilia na si kila kitu.

5. Hisia zilizofichwa

Kuna watu huwa wanadhani furaha ya maisha iko kwa watu ambao wanayo hiyo furaha hivyo kwamba wao huwa hawakasiriki. Hiyo si kweli kila mtu ana hisia sawa, utofauti unakupa ni namna gani tunaonyesha kuwa na furaha hiyo. Kwa lugha nyingine watu wenye furaha wakikasirika huwa hawafichi hasira zao, hivyo utajua tu lakini hiyo itapita.Hivyo unapojaribu kutokuonyesha hisia zako kama hasira ni vigumu kuondoka, itaongezeka na kuongezeka. Lakini ukionyesha hasira zako na kushungulika nazo zitaondoka na kuruhusu furaha itawale maisha yako tena.

6. Kujizungushia ukuta

Unapokuwa umejifungia ndani peke yako si rahisi kujua kitu gani kinaendela nje ya kuta zilizokuzunguka. Si kwa bahati nzuri ila utagundua watu wenye furaha hupenda kuchanganyika kwenye mambo mengi ya kifamilia, kusafiri na hata mijumuiko ya kijamii. Jinsi unavyokaa peke yako ndivyo inavyokuwa ngumu kutoka hapo ulipo, unahitaji kukutana na watu wengine ili ujue vitu vinavyokwenda na kujiondoa kwenye hatari ya kuwa na mongo wa mawazo.

7. Kuwa na matarajio mengi kuliko kawaida

Pale inapotokea una matarajio mengi na hayafanikiwi unapata mawazo mengi. Usitegemee kila mtu kufanya vitu kama vile wewe unavyotaka kila mtu ana mtazamo wake wa maisha. Hivyo si kila wakati utataka mambo yaende unavyotaka wewe. Kuachana na matarajio mengi haimaanishi uruhusu mambo yaende vibaya, hapana ila unaruhusu mambo yanende vile yalivyo na vile yanavyotakiwa kuwa.

8. Kukaa kwenye kazi unayoichukia

Ni vigumu kuwa na furaha kama unatumia masaa 40 kila wiki katika kazi ambayo unaichukia. Na ni vigumu pia kufurahi kama kazi hiyo huwezi kuiacha. Ila kama huipendi kazi hiyo sasa unaweza kuanza mchakato wa kubadirisha kazi au taaluma kwa kuanza kuweka akiba ya kukusaidia kuondoka hapo na kuelekea mahali pengine. Ni kawaida kutoipenda kazi na miaka 20 baadaye ukajikuta uko kwenye kazi hiyo hiyo.

9. Kuwa mlalamishi sana

Watu wajinga siku zote huleta utata hata katika vitu vya msingi, kuhukumu bila sababu na kulalamika sana. Ingawa kulalamika wakati mwingine kunaruhusiwa na kunakubalika. Itakuwa vizuri kuiondoa kila kitu kifuani na kuruhusu kitoke kwako lakini tabia ya kulalamika kila wakati inakuharibia mwonekano wako na namna watu wanavyokuchukulia.

10. Kuwadharau watu wengine na kupenda visasi

Kuna watu wanafikiri wakidharau watu wengine wanajisikia vizuri na hiyo ndipo furaha yao. Hiyo inakupa furaha na kujisikia vizuri kwa muda mchache tu ila utakaa muda mrefu utajikuta wewe ni yule yule, hata ukidharau watu wengine huna uwezo wa kuzuia ndoto zao. Hivyo na wakati mwingine unajikuta una kinyongo na watu na unajitengenezea visasi. Huwezi kuwa na furaha katika harakati zako kwani wakati wote uko katika kupambana na watu kwenye fikra zako.

Kuwa na furaha ni maamuzi ambayo unaamua kuyafanya ili uwe mwenye afya na akili iliyotulia inayoweza kutekeleza majukumu yake sawa sawa. Ingawa kuna wengine hawana furaha kwa sababu ya uoga wa kuogopa amisha ya baadaye hiyo wana wasiwasi sana na kushindwa kufurahia maisha ya sasa. Kuna sababu nyingi ila je unazishughulikiaje ili zisikuondolee furaha kwenye maisha yako?

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents