Habari

Upinzani nchini Kenya waitaka tume ya uchaguzi imtangaze Raila Odinga mshindi

Muungano wa upinzani nchini Kenya (NASA) umeendelea kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais yanayotangazwa na tume huru ya uchaguzi nchini humo (IEBC) huku umoja huo ukitaka tume imtangaze kiongozi wao Raila Odinga kuwa mshindi.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga

Viongozi wa muungano huo wamesema walikutana na wakuu wa Tume ya Uchaguzi na kuwasilisha rasmi malalamiko yao kupitia barua.

Msemaji mkuu wa upinzani, Musalia Mudavadi amabaye aliwahi kuwa naibu waziri mkuu, amesema upinzani umepata maelezo zaidi kwamba matokeo ya uchaguzi yalivurugwa baada ya kudukuliwa kwa mitambo ya IEBC.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo, Wafula Chebukati amekanusha taarifa hizo kwa kusema kulikuwa na jaribio la kudukua mitambo hiyo, lakini halikufanikiwa.

Bw Mudavadi amedai mgombea wa upinzani Raila Odinga ndiye aliyeshinda uchaguzi huo mpaka sasa na tayari ameitaka tume kumtangaza Raila Odinga.

“Twamtaka mwenyekiti wa IEBC atangaze matokeo na kumtangaza Odinga na Kalonzo rais mteule na naibu rais mteule wa Kenya mara moja”,amesema Bw Mudavadi kwenye mkutano na Waandishi wa Habari leo.

Kwa mujibu wa sheria nchini Kenya ni kosa mtu yeyote kutangaza matokeo au kusambaza matokeo ambayo hayajatoka katika tume ya taifa ya uchaguzi kwani tume ndio ina mamlaka ya kutangaza matokeo.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents