Burudani

Vanessa Mdee aja na #VeeXperience kuwashukuru mashabiki wanaompigia kura zaidi

Vanessa Mdee anarudisha fadhila kwa mashabiki wake kwa namna ya kipekee. Amekuja na kitu alichokipa jina #VeeXperience.

Photo Jun 18, 1 30 39 PM

“Nimeona kwasababu ya hii nomination, mimi naona tushiriki pamoja, not only kwa kupiga kura but to experience different things na mimi. Kwahiyo kwa wiki nne nitafanya #VeeXperience mpaka siku hiyo ya tuzo,” Vanessa ameiambia Bongo5.

“Last week ilikuwa #DinnerWithVee ambayo ilikuwa surprise dinner, shout outs to my fans ambao walishinda, wasichana wawili wazuri ambao walikuja kupata dinner na mimi nikawasurprise Jux akawepo, Navy Kenzo wakawepo. Ilikuwa ni shukrani kwa wale ambao wamehamisha wenzao kupiga kura za KTMA na hapa tunapoanza sasa safari ya MAMA hao hao wanakuwa wanatusaidia,” ameongeza Vee.

“This week is a #PhotoShootWithVee. So shabiki mmoja atapata chance ya kufanya photoshoot na mimi na @ossegrecasinare who is an amazing photographer. Osse pia anatengeneza graphics, he is just amazing, mimi nataka kusogea na watu. Na hizi picha utakuwa nazo, utabaki nazo forever, ni zaidi ya selfie hata. Next week tuna #CampusInvasion siwezi kusema zaidi but it’s a #VeeXprience I can’t wait for you to see it.”

Vanessa amesema nafasi hiyo itaenda kwa shabiki atakayehamasisha watu wengi zaidi kumpigia kura za #MTVMAMA2015 kwa kutumia hashtag #VeeXprience au #PhotoShootWithVee kwa wiki hii.

“My team is looking out for everyone who uses the hashtag and they get a chance to win.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents