Vanessa na Jux waandika historia kwenye muziki wao Mtwara (Picha)

Tamasha la muziki la In Love&Money Tour la muimbaji Vanessa Mdee pamoja na mpenzi wake Jux limeendelea kufanya vizuri baada ya usiku wa jana mkoani Mtwara kufanya show ya nguvu na kujaza uwanja.

Umati wa mashabiki uliojitokeza kwenye tamasha hilo.

Wawili hao wamefanya tamasha hilo kwa mara ya pili baada ya tamasha hilo kufanyika kwa mafanikio kwa mara ya kwanza mkoani Mwanza.

Wasanii wengine ambao walionyesha support kwenye tamasha hili ni rapa Joh Makini, Chege, Ben Pol, Barnaba, Mario pamoja Mimi Mars.

Baada ya tamasha hilo kumalizika kwa mafanikio, Vanessa alimshukuru Mungu huku akiwataka wasanii wengine kujaribu kufanya vitu kama hivyo licha ya kukatishwa tamaa.

“BWANA NI MCHUNGAJI WANGU SITAPUNGUKIWA NA KITU. Na kama mchungaji amekupa kibali kufanya jambo lolote, usimruhusu mwanadamu akukatishe tamaa, ng’ang’ana ili kusudi lake litimie! Asante Sana Sana Sana MTWARA,” aliandika Vanessa kupitia Instagram.

Naye Jux aliongeza, “We did it again Baby @vanessamdee Kwanza kabisa namshukuru Mungu pia wasanii wenzangu kwa support mliotupa tena @johmakinitz @gnakowarawara @nikkwapili @chegechigunda @iambenpol @barnabaclassic @marioo_tz @djzero @mimi_mvrs11 @_nancyhebron @masseur_cerebral @kreestofficial mnyama makali @lilommy wa mwisho kabisa @freconic_ideaz kwakuweza kukamilisha zoezi hili bila kusahau #afjproductions na @cloudsplus kwa kuwezesha watu wa nyumbani kuona show live kabisa Asante @pridefmtz #inloveandmoneytour MTWARA MMETISHA SANA,”

Wawili hao bado hawajatangaza tamasha hilo litaelekea mkoani gani baada ya kufanyika kwa mafanikio katika mikoa hiyo miwili.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW