Habari

Video: ACT – Wazalendo wanena mazito baada ya viongozi wao kung’atuka

Baada ya kujiuzulu Mwenyekiti wa kampeni na uchaguzi,Samson Mwigamba wa chama cha ACT- Wazalendo , Chama hicho kimeeleza kuwa kina utamaduni wake na hawatauwacha utamaduni huo wa kuheshimu mawazo ya mtu hivyo wanaheshimu mawazo ya kiongozi huyo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi, Ado Shaibu amesema kuwa Mwigamba bado ni mwanachama wa Chama hicho na ana haki zake na anao wajibu wake wa uanachama.

“Samson Mwigamba amejiuzulu nafasi yake kama Mwenyekiti wa kampeni na uchaguzi waandishi wanasema na ww umesema kwamba tuko zaidi sana na Chama cha Mapinduzi na mengineyo wanayaandika mimi niseme jambo moja kuhusu suala hili suala la ndugu Mwigulu kuna nukta mbili sana mtuelewe, chama cha ACT – Wazalendo kinao utamaduni wake na hatutaacha utamaduni wetu tulioujenga kwa miaka mitatu ya uwepo wetu moja tuna heshimu maamuzi ya mtu hatumshinikizi mtu kwahiyo katika hilo tunaheshimu maamuzi ya ndugu Mwigamba kukaa pembeni katika uongozi jambo la pili ambalo ni utamaduni pia tunaheshimiana,” amsema Ado Shaibu.

“Kwahiyo ndugu Mwigamba bado ni mwanachama wa Chama chetu kwahiyo anazo haki zake na anao wajibu wake wa uanachama yupo pamoja nasi kwahiyo tuna mheshimu hayo mambo mawili mpaka itakapo kuwa vinginevyo kwa mfano tukiona sasa hatuheshimiani kwa maana yake kuheshimiana ni jambo la pande zote mbili.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents