Burudani

Video: Baby J adai hana mpinzani kwenye muziki

Msanii wa muziki kutoka Visiwani Zanzibar, Baby J amefunguka kuwa hana mpinzani katika muziki anaoufanya.

Akiongea na Bongo5, Baby ameeleza kuwa hajawahi kuwa na mpinzani katika muziki anaofanya yeye, Licha ya kuwa miaka ya zamani alikuwa akishindanishwa na mwanamuziki Sainaj kutokea huko huko, mrembo huyo amekana kuwa na mpinzani.

“Kwanza sijawahi kuwa na mpinzani, kwa sababu siku zote unakuwa unajiona wewe mwenyewe huoni cha mbali mimi navyo jiona yani kwanza nime zaliwa Zanzibar, nimefumbua macho Zanzibar, hao wote wanaojiita wapinzani ndiyo nimewepokea hapa Zanzibar, so siamini kama nina mpinzani,” amesema mrembo huyo ambaye hivi karibuni ameshirikishwa kwenye ngoma mpya ya Kasssim Mganga.

Pia ameongeza kuwa moja ya sababu zinazowafanya wasanii wa kike kuwa wa chache kisiwani humo ni kutokana na kutokujiamini.

Na Laila Sued na Salum Kaorata

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents