Burudani

Video: Huyu ndio rapper atakaye sikika katika ngoma mpya ya Baby J

Baada ya ukimya wa mrefu katika muziki, hatimaye msanii wa Bongo Flava, Baby J amedai kuwa anatarajia kuachia ngoma yake mpya hivi karibuni.

Akiongea na Bongo5, Baby J ameeleza kuwa hivi karibuni anatarajia kuachia ngoma yake mpya aliyomshirikisha mkali wa Hip Hop Bongo, Mwana FA.

“Nina ngoma kali sana sijawahi kujisifia ,nimepata confidence sana kuongea hivi kwa sababu watu nilio wasikilizisha wanajua muziki na wapo kwenye industries kitambo tangu mie nasoma yah, nina comfidence ndiyo maana naweza kusema hivyo na nimefanya ngoma yangu na Mwana FA,” amesema mrembo huyo.

Pia msanii huyo ameongeza kuwa ngoma hiyo itakuwa katika mahadhi ya reggae, na sio maahdhi ya pwani kama watu walivyo mzoea katika ngoma zingine.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents