Habari

Video: Lissu anajitambua – Dk. Mashinji

Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt Vincent Mashinji amesema kuwa aepokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti Mkuu wa Chama hicho kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anaendelea vizuri na anajitambua.

Akizungumza na Wanahabari leo, Dk Mashinji amesema tukio hilo lililomtokea Mbunge huyo ni la kusikitisha sana na kufedhesha.

“Mhe. Tundu Antifas Lissu Mbunge wa Singida Mashariki mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni ni Rais wa watetezi wa haki ni Rais wa wale wote wanaopenda haki itendeke kwahiyo ukisimama ukitaka kuzungumzia suala la haki Rais wake ni Tundu Antifas Lissu jana akiwa anatoka bungeni kuna gari ilimfuata alipokuwa akifika nyumbani kwake walimmiminia risasi za kutosha kama vile wanashambulia mnyama mkali asie na utu na binadam, tukio hili lilikuwa ni la kusikitisha sana na kufedhesha,” alisema Dk Mashinji

“Tunawashukuru wote waliokuwa katika eneo la tukio kwasababu cha kwanza walichokikumbuka katika akili yao ni kuokoa maisha ya Chama wa wanasheria Tanzania (TLS), alipelekwa hospitali ya Dodoma tunawashukuru sana madaktari wa hospitali ya Dodoma kwa jitihada zote walizozifanya kuokoa maisha yake na mpaka asubuhi ya leo Tundu Lissu tuko nae hai najisikia kidogo niko protected kwasababu na mimi nina advantage ya hiyo professional ni daktari pia na sio daktari tu nilisoma emergence medicine na hii ni hatua ya kwanza ambapo unamtengeneza mgonjwa kabla madaktari wengine hawajaanza kumtibu kwahiyo ni washukuru madaktari wa hospitali ya Dodoma na watu wote Mungu awabariki sana waendelee na moyo huo huo.”

“Tundu Lissu alifika Nairobi asubuhi hii na mpaka sasa wa Chama anasema ameachana nae akiwa anajitambua, Mwenyekiti amewapa salam na pole na amesisitiza makamanda tuendelee kupambana na taifa letu,” Alieleza huku akishangiliwa na wafuasi wa chama hicho.

Hata hivyo Dkt Mashinji amewahasa wanachama hao kuhakikisha wanachangia damu kuhakikisha benki za damu zinakuwa na damu ya kutosha ili ziwasaidie wahitaji.

Na Salum Kaorata

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents