Video: Msanii Dogo Richie aandika historia mpya Kenya kwa hili!

Unapokua nchini Kenya, jina Bin Laden lina maana tofauti kabisa na vile pengine wengi tumezoe kuwa lina linganishwa na ugaidi.

Lakini msanii matata wa nchini Kenya ambae amekua akiangaziwa na vyombo vya habari nchni humo kwa hulka yake ya kuwachamba wanasiasia na wasanii wenzake ambao anahisi wanapotosha umma kwa kutumia njia za mkato kujilimbikizia mali ama kushiriki tabia za kifisadi. Hali ambayo ilimfanya kutengwa na waandaji wa matamasha ya kiserekali.

Jana kwa mara ya kwanza baada ya mda mrefu kuwekwa benchi na waandaji wa matamasha haswa kwenye jimbo la Mombasa, Dogo Richie alipanda jukwaani kwenye tamasha la kusherehekea siku ya utalii duniani. Kwa hamu na gamu mashabiki walisubiri kufika kwa zamu ya nyota huyu wa muziki, ambaye kwa jina la msimbo anajiita Bin Laden, kwa kua anaamani yeye kwahivi sasa ameiva na hata umaarufu wake umepanda. Na kweli alipo panda jukwaani mashabiki walipagawa na kuimba nyimbo zake zote alizoimba kwenye jukwaa. Chini hapa ni video ikionyesha jinsi Dogo Richie alovyowaimbisha mashabiki wake.

Imeandikwa na muandishi Changez Ndzai- Kenya

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW