Burudani

Video: Nahreel asimulia jinsi rapper K.O alivyopagawa na midundo yake, anafanya kazi pia na AKA

Producer Nahreel hakushinda tuzo ya mtayarishaji bora wa Bongo Flava kwenye KTMA 2015 kwa kubahatisha kwakuwa sasa rappers maarufu wa Afrika Kusini wakiwemo K.O na AKA wamedata na uwezo wake.

Nahreel amesema anatayarisha ngoma za rappers hao walio kwenye top five ya wasanii wa hip hop wanaokiki nchini humo.

“Wakati tumeenda SA tulikutana na wasanii wengi kama K.O, AKA, akina Muggz ile Cashtime nzima na K.O ana album yake inakuja, anafanya collabo yeye na AKA, sijajua itatoka lini lakini nilimpatia beat tatu. Wakati tupo pale studio tulikuwa na ile break time nikapiga zile beat kwahiyo akatokea kuzipenda sana,” amesema Nahreel.

“Alikuwa nje akasikia akaja [K.O] akauliza ‘hizi beat za nani?’ nikasema zangu, akasema ‘man the beats are sick we need to talk’, akanivuta hapo hapo pembeni. Kwahiyo akasema ‘Nahreel hizi beat lazima unipatie nina album yangu mimi nafanya na AKA. Na juzi wakati AKA anafanya press conference na MTV MAMA akataja, waandishi wa habari wengi walikuwepo walisikia akasema, ‘I am working with the biggest producer now Nahreel from TZ in a new coming project’, kwahiyo hiyo ni kazi ambayo naitegemea itakuwa nzuri kwasababu the beats are really good,” alisisitiza Nahreel.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents