Burudani

Video: Nazizi akanusha kuachana na mume wake kwa lengo la kuvuna mali

Rapper wa kundi la Necessary Noize la Kenya, Nazizi amekanusha shutuma kuwa aliachana na mume wake wa miaka mitano ili avune mali walizokuwa wanamiliki.

https://www.youtube.com/watch?v=vE9rvomd720

Akiongea kwenye kipindi cha The Trend cha NTV ya Kenya jana, Nazizi alidai kuwa kwanza mume wake huyo kutoka Tanzania si tajiri wa Mombasa kama baadhi ya watu wanavyodai.

Alisema kuwa waliachana kwa sababu waligundua kuwa hawakuwa na muda wa kutosha kuwa pamoja kwakuwa mara nyingi walikuwa ni watu wa kusafiri na kwasababu wote wanampenda mtoto wao wa kiume walilazimika kuokoa ndoa yao japo ilifika sehemu wakaona haiwezekani.

Wawili hao walinununua kiwanja pembezoni na bahari huko Lamu nchini Kenya na alidai kuwa taraka yao ya kiislamu ambayo imetoka tayari haitahusisha masuala ya kugawana mali.

“Hakuna anayepata chochote, hapati changu, nami sipati chake chochote, tulichokuwa tunataka wote ni mtoto wetu awe na maisha mazuri” alisema Nazizi.

“Kama ningekuwa nimeolewa na mwanaume tajiri nisingeomba taraka… hapana, natania tu.. lakini sio kweli.”

Rapper huyo pia jana alitambulisha wimbo wake mpya 254 (Born and Raised in Nai) ambao ni wa kwanza kutoka kwenye album yake mpya ‘Evolussion’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents