Habari

Video: Ray azungumzia movie zake mpya 3 na namna mazoezi yalivyobadilisha afya na muonekano wake

Vincent Kigosi aka Ray yupo kwenye dilemma. Ana movie tatu mpya na kwa mujibu wake, zote ni kali ila hajui aanze kutoa ipi.

“Nina movie kama tatu, sijajua naanza kuitoa ipi, nina VIP, Add Price na Chicken Head. Mpaka sasa sijajua ntaitoa movie gani, tukikaa kama uongozi wa RJ Company tutajua tutatoa sinema gani baada ya kutoka Fans of Death ambayo mwisho wa mwezi huu,” alisema Ray.

Kuhusu filamu ya Sister Marry iliyozuiliwa kutoka na bodi ya filamu Tanzania mpaka iondolewe scene zenye utata, Ray amesema japo wameshafanya marekebisho waliyotakiwa kuyafanya, hawataitoa muda huu kutokana na hali ilivyo nchini kwa sasa.

“Kutokana na masuala ambayo yapo sasa hivi katika nchi yetu ya udini udini mwingi, tukasema kwanza hebu tuache ipumzike kidogo lakini tutakuja kuitoa baadaye.”

Katika hatua nyingine Ray amesema mazoezi yamemsaidia kwa kiasi kikubwa kwakuwa awali alikuwa ameanza kunenepa na mwili kuanza kumshinda.

“Ukishakuwa muigizaji, mtu ambaye unaonekana mara kwa mara lazima utengeneze good looking yako, muonekano wako uwe mzuri,” alisema Ray na kuongeza kuwa tangia alipoanza kufanya mazoezi afya yake ni nzuri na kila nguo inampendeza.

“Mazoezi unajenga mwili, unakuwa na mwili mzuri, unavaa nguo yoyote unayoitaka. Sasa nacheza kama mwanafunzi, nikicheza kijijini nacheza, lakini zamani siwezi kucheza kama mwanafunzi na kitambi kama pipa bwana.”

Ray ameshawauri waigizaji wenzie hususan JB na watu wa kawaida wafanye mazoezi kwakuwa ni muhimu katika mwili wa binadamu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents