Burudani

Video: Ray C aonjesha nyimbo zake mbili mpya

Rehema Chalamila aka Ray C, yupo studio ambako anaendelea kurekodi nyimbo mpya. Muimbaji huyo mwenye sauti tamu na aliyekuwa akisifika kwa kiuno chake kisichokuwa na mfupa, ameshare video kwenye mtandao wa Instagram wa nyimbo zake mpya.

Moja ya video hiyo unasikika wimbo wake wenye mahadhi kama ya taarab huku akiimba ‘binadamu ni wabaya, sura zao hazina haya, mambo yanatunyookea, issue zetu ziko sawa’.

Na video nyingine inamuonesha Muki, wa kundi la Makomando akicheza wimbo uliochangamka kiasi unaonekana ameshirikishwa na Ray C.

Unadhani nyimbo hizo zinaweza kumrudisha kwenye chart?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents