Burudani

Video: Ruby azungumzia muziki wake na kile atakachokifanya kesho kwenye show yake katika Tuzo za Watu

Ruby anaendelea kufanya vizuri na wimbo wake ‘Na Yule’ na tayari ameshatoa video ya wimbo huo.

Muimbaji huyo mwenye sauti ya kipekee na mwenye kipaji kikubwa atatumbuiza Ijumaa hii kwenye Tuzo za Watu zitakazofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

“Watu wategemee performance nzuri kutoka kwangu,” amesema Ruby. “Kama kawaida mimi napenda muziki mzuri na itakuwa ni live performance. So wategemee kizuri na hali ya hewa ya muziki na yenyewe itabadilikabadilika kutoka kwa Ruby.”

Katika hatua nyingine Ruby amesema uwezo wake wa kuimba live ni kutokana na kuimba sana muziki wa gospel kabla ya hapo alipo leo.

Amesema kutokana na kuwa mtu wa kanisa zaidi ilimwia vigumu kuweza kueleweka kwa watu wake wa karibu ambao wapo waliomtenga.

Mtazame zaidi kwenye video hiyo juu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents