Habari

Video: Serikali itagharamia matibabu ya Tundu Lissu endapo…- Waziri Ummy

Waziri wa Afya, Maaendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema serikali iko tayari kugharamia matibabu ya Tundu Lissu na kumhudumia popote anapotaka kupelekwa duniani endapo itapata maombi rasmi kutoka kwa madaktari bingwa pamoja na familia yake.

Waziri Ummy akizungumza na wanahabari jijini Tanga leo, amesema serikali inashangazwa kuona watu wanachangishana mitandaoni kana kwamba serikali haipo, hivyo kwa upande wao wanaona kuwa jambo hilo limegubikwa na mambo ya kisiasa.

“Kuhusu matibabu ya Mhe. Tundu Lissu Mbunge wa Singida Mashariki ndicho kilichonifanya niongee nanyi, kutaka kutoa ufafanuzi kwa Watanzania lakini pia kwa familia ya Ndugu Lissu, tunaona kuna taarifa zinapotoshwa lakini pia kuna mambo mbalimbali yanafanywa ambayo hatujui haswa lengo lake nini kama mnavyofahamu Septemba 7, 2017 alipelekwa katika hospitali ya rufaa ya Dodoma na akiwa na majeraha sehemu mbalimbali mwilini, kufuatia shambulio ambalo amelipata la risasi katika makazi yake eneo la Dodoma na alipofikishwa katika hospitali yetu ya rufaa ya Dodoma alikuwa na hali mbaya na inabidi apelekwe chumba cha upasuaji cha theatre ,” amesema Waziri Ummy.

“Serikali ipo tayari kumuhudumia Mhe. Tundu Lissu popote anapotaka kupelekwa duniani as long as tutapata maombi kutoka kwa familia mpaka dakika hii hatujapata maombi rasmi kutoka kwa familia endapo sasa hivi tutapata maombi rasmi kutoka kwa familia ambayo yataambatana na taarifa za madaktari ya kwamba muheshimiwa Lissu anahitaji huduma za matibabu ya kibingwa zaidi tupo tayari kufanya hivyo mara moja kama serikali,” aliongeza.

“Serikali haijakataa na wala haijashindwa kumhudumia Mhe. Tundu Lissu, Mhe. Tundu Lissu ni Mtanzania na nyie wenyewe ni mashahidi kama kama kuna Mtanzania tu wa kawaida serikali ina gharamia matibabu yake pale inapohitajika, hatuwezi kufanya hivyo kwa Tundu Lissu kwasababu yeye ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents