Habari

Video: Tusiilaumu Serikali kwa ukosefu wa ajira

By  | 

Wanafunzi wa Shirikisho la Vyuo Vikuu Nchini wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wanaomaliza masomo yao wametakiwa kuacha kukichukia chama hicho kwa madai ya kukosa ajira kwani kufanya hivyo nikwenda kunyume na ilani ya chama.

Hayo yamezungumzwa na Mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana(UVCCM) Taifa, anaewakilisha mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Siluti wilaya ya Namtumbo Halfan Kigwenembe katika mahafari ya pili ya shirikisho la vyuo vikuu mkoa wa Ruvuma.

“Kwani tusiilaumu Serikali kwa ukosefu wa ajira,mimi leo ningeinga’nga’nia ajira serikali nisingekuwepo hapa, nilikuwa na uwezo wa kuipata lakini kwasababu nina uwezo wa kuipata basi niinga’nga’nie, mimi nikae pembeni nipishe wasiokuwa na uwezo wa kuipata waipate, kwahiyo mimi nawaombeni sana na ndio wito wangu kwenu tuangalie source na fursa za kujiajiri,” alisema Kigwenembe.

Video:

Na Emmy Mwaipopo

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments