Habari

Viongozi wa dini waombwa kuliombea taifa amani

Naibu waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo, Anastazia Wambura,amewaomba viongozi wa dini na waumini wa madhehebu yote nchi kushirikiana kuliombea taifa liendelee kuwa na amani na utulivu.

1471174090-anastazia-wambura

Ametoa wito huo jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushiriki kongamano maalum la kuombea taifa amani linaloandaliwa na Kalismatic Catholic jimbo kuu la Dar es Salaam.

Akiwa kama mgeni rasmi amesema licha ya taifa kuwa na amani bado linahitaji maombezi hayo ili tunu hiyo iwe endelevu kwa maendeleo ya taifa.

“Kwanza kabisa tunachohitaji ni amani na sio serikali peke yake ina mahitaji haya, kila mwananchi anahitaji amani, kwasababu bila amani hakuna kitu chochote ambacho kinaweza kikafanyika, hakuna kazi yoyote ya maendeleo wala shughuli zozote za binafsi zinazofanyika kama hakuna amani. Kwasababu tumeweza kushuhudia ambapo kikitokea tu kitu kama haya matukio ya athari watu wamekuwa wakikimbia huku na kule,kwahiyo kimsingi amani ndicho kitu cha kwanza,” alisema.

Viongozi mbalimbali wa serikali ya awamu ya tano akiwepo Rais John Magufuli, wamekuwa wakisisitiza amani na kuendelea kuwaomba viongozi wa dini nchini kuliombea taifa amani.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents