Michezo

Vita ya Mourinho vs Guardiola, Rekodi zinaibeba Manchester United

Kocha wa klabu ya  Manchester United, Jose Mourinho na mwenzake Pep Guardiola wa Manchester City wataoneshana ubabe leo watakapokutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu nchini England.

Mchezo huo wa ligi kuu soka ya EPL utapigwa katika dimba la Old Trafford majira ya saa moja jioni ambapo Manchester United ina rekodi ya kutopoteza mchezo hata mmoja katika mechi 40 mfululizo katika uwanja huo.

Timu hizo mpaka sasa zimekutana mara 144 ambapo Man United imeshinda mechi 72, Man City ikishinda mechi 50 tu huku mechi 52 wakitoa sare.

Hata hivyo pamoja na kuwa na rekodi hiyo lakini timu ya mwisho kuifunga Manchester United katika uwanja wake wa nyumbani ilikuwa ni Man City na ilikuwa msimu uliopita katika mchezo uliopigwa Septemba 2016.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents