Habari

Vyama 7 vilivyojitoa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa vyatoa tamko jipya

Siku moja kabla ya kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuanza vyama saba vilivyojitoa katika mchakato wa uchaguzi huo vimetoa tamko vikiwataka Watanzania kujiandaa kwa maelekezo mengine yatakayotolewa baada ya kumalizia mashauriano.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Novemba 16 baada vyama vya Chadema, ACT-Wazalendo, Chaumma, CCK, NCCR Mageuzi, UPDP na NLD kutoa msimamo wao.

Akiongea kwa niaba ya vyama hivyo, Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari amesema vyama hivyo vilishatoa matamko ya kujitoa kwenye uchaguzi huo kutokana na ukiukwaji wa kampuni na sheria.

Amesema baada ya vyama hivyo kujitoa kushiriki uchaguzi, serikali kwa upande wake ilitoa matamko mbalimbali yaliyokuwa yakitofautiana na kuchanganya, licha ya kuwa yalikuwa yakitolewa na mtu mmoja ambaye ni Waziri wa Tamisemi.

“Baada ya wagombea wa vyama hivyo kujitoa kwenye uchaguzi huo, waliwajulisha wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kuhusu kujitoa na kwa ngazi ya Taifa baadhi ya vyama vilimjulisha waziri wa Tamisemi kwa barua,” amesema Profesa Safari.

Baada ya kushauriana vyama hivyo vimeazimia kwa pamoja havitashiriki kwa vyovyote “kwenye kampeni na uchaguzi unaoenda kinyume na kanuni za uchaguzi” na vimewataka wanachama na wafuasi kutoshiriki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents