Habari

Wabunge 10 wa CUF wanaomuunga mkono Seif Hamad wasusia kikao

Kwa kile kinachoonekana kama kususia Kikao, Wabunge 10 na madiwani wawili wa Chama cha Wananchi (CUF) walioitwa leo kwa ajili ya mahojiano katika Ofisi za Chama hawajatokea .

Makao makuu ya CUF

Wabunge hao wanaomuunga mkono, Katibu Mkuu wa CUF, Seif Shariff Hamad waliitwa ili kuhojiwa na Kamati ya Nidhamu na Maadili ya chama hicho kuhusu mgogoro unaoendelea.

Katika taarifa iliyotolewa jana na chama hicho upande unaomuunga mkono, Mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba uliwataka viongozi hao kufika katika ofisi hizo saa 3.00 asubuhi leo lakini mpaka kufikia saa 6:00 mchana walikuwa bado hawajafika.

Mbunge wa viti maalum wa chama hicho aliyeitwa kwenye mahojiano hayo, Severina Mwijage amesema hana taarifa za kuitwa kwenye kikao hicho.

Niko safarini Bukoba sifahamu kuhusu kuwepo kwa kikao hicho,” amesema Mhe Mwijage kwenye mahojiano yake na Gazeti la Mwananchi.

Mbunge mwingine wa viti maalum wa chama hicho, Mgeni Kadika amesema alipata taarifa za kuwepo kwa kikao hicho lakini hatahudhuria.

Nilipata taarifa kupitia ujumbe mfupi (SMS) lakini sitafika kwenye kikao hicho kwa kuwa nauguliwa na watoto huku Pemba,” amesema Kadika.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents