Habari

Wabunge watahadharishwa usalama wao

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewatadharisha wabunge kuwa makini na usalama wao ikiwa ni pamoja na kutokaa baa usiku wa manane.

Spika Ndugai ameyasema hayo leo Ijumaa kabla ya kuahirishwa kwa Bunge,amewataka kutokaa sana katika mabaa na wawahi nyumbani.

“Waheshimiwa wabunge niwaase tu kuhusu usalama wetu, kwamba tuwe makini na usalama wa maisha yetu na tusijiachie sana tuwapo katika majimbo yetu ama mahala pengine tunapoenda. Tusikae kwenye mabaa hadi usiku wa manane. Usalama unaanza na wewe mwenyewe”, amesema Spika Ndugai

“Yaani tuchukue hatua tu katika maisha yetu kama mnavyosikia matukio ni mengi katika nchi yetu. Ni vizuri usalama unaanza na wewe mwenyewe kwanza,”amesema.

Septemba 7, mwaka huu Mbunge wa Singida Kaskazini Tundu Lissu alijeruhiwa kujeruhiwa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake ‘Area D’ mjini Dodoma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents