BurudaniVideos

Wafahamu OMG – Kundi la rap linaloiteka Tanzania kwa kishindo (Video)

OMG au OH MY GOD ni kundi la rap la vijana watatu – Young Lunya, Salmin Swagg na Con Boi ambalo tayari limeanza kutengeneza vichwa vya habari kutokana na uwezo wake wa kipekee.

12501682_844661322309818_1662583209_n

Hawasifiki kwa style za rap ya kisasa tu bali pia uandishi wao umeshiba kiasi cha kuwatofautisha na rappers wengi wapya. Wanasema walikutanishwa pamoja na Mesen Selekta huku Conboi akitolewa kutoka kwao mjini Morogoro.

Walikuja kukutana na producer wa Switch Records, Lufa ambaye wanasema wanaendana naye zaidi kutokana na aina ya muziki wao. Hadi sasa wameachia kazi mbili, FIT na D.O.D.

Wanasema muziki wao ambao umelalia kwenye trap music umewafanya wapate mashabiki wengi ‘teenagers.’ Hata hivyo wanasema uwezo wao unawapa nafasi ya kufanya kila aina ya muziki.

Wafahamu zaidi kwa kutazama interview yao hapo juu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents