Habari

Wafungwa 35 wauawa kikatili Gerezani

Gavana wa jimbo la Amazonas nchini Venezuela, Liborio Guarulla amesema zaidi ya wafungwa 35 wameuawa kwa kupigwa risasi gerezani katika kile kilichoitwa ‘Mauaji kwa watumiaji madawa’ kinachotekelezwa na maaskari nchini humo.

Waandishi wa Habari waliokusanyika nje ya Gereza hilo leo usiku kufuatilia tukio hilo lililotokea jana

Kikosi maalumu cha jeshi cha wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo leo Agosti 17  kimepelekwa kudhibiti hali ya ndani ya gereza katika mji mkuu wa jimbo hilo, Puerto Ayacucho.

Taarifa kutoka shirika la habari la AFP zinaeleza kuwa Watu waliokaribu na gereza hilo walishuhudia tukio hilo kwa kusema walisikia milio ya risasi kwa saa kadhaa na vilio, ingawaje mpaka sasa hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na Serikali.

Asasi nyingi za kiraia nchini humo na zile za kimataifa zimekuwa zikilaumu uongozi wa Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro kwa kutokuzingatia haki za binadamu baada ya kutekeleza mauaji dhidi ya watu wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya ikiwemo wafungwa ambao walihukumiwa kwa makosa kama hayo.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents