Habari

Waigizaji wa filamu 10 wa kike matajiri zaidi nchini Nigeria

Kate Henshaw – Nuttall

Hawa ni wasanii kumi wa kike wa Nollywood wanaoingiza fedha nyingi zaidi kwa uigizaji, matangazo na biashara na shughuli walizojihusisha nazo miaka kadhaa iliyopita.

1. Kate Henshaw-Nuttall – Naira milioni 67 (TSH 674,266,580)

Mpaka mwaka 2006, alikuwa ameshaingiza Naira milioni 10 na mwaka uliofuatia alifikisha Naira milioni 12. Muigizaji na model huyo alikuwa balozi wa mtandao Glo Ambassador na sura ya Onga. Mwaka 2008 – 2010 aliingiza takriban Naira milioni 20.

2. Genevieve Nnaji – Naira milioni 64 (TSH 644,075,940)

Muigizaji huyu mrembo mwaka 2009 alilipwa dola 25,000 kuigiza kwenye filamu ya kimataifa ya ‘IJE’. Mwaka 2004 model na muimbaji huyu aliteuliwa kuwa kisura wa Lux pamoja na kufanya matangazo ya kinywaji cha Pronto na sabuni ya Omo.

Kati ya mwaka 2004 hadi 2006 aliinguza naira milioni 31.3.

Naira milioni 14.7 alizipata kutokana na mchongo wa Lux ($100,000). Mwaka 2008 alianzisha mavazi yake ya St. Genevieve ambazo kitega uchumi chake kinakadiriwa kuwa na thamani ya NAIRA milioni 20.

June 15 mwaka huu aliteuliwa kuwa balozi wa Range Rover Evoque nchini Nigeria, mchongo ambao ulimpa pesa ya kutosha.

3. Ini Edo – Naira milioni 60

Mrembo huyu ana mijengo mitano ya nguvu na nyingi amezipangisha. Mwaka 2007 alikuwa ameshaingiza Naira milioni 15.7 kutokana na movie na biashara zake.

Kwa sasa ana deal na mtandao wa Glo.Mara nyingi anahusika na Nollywood USA.

4. Rita Dominic – Naira milioni 58


Muigizaji huyo ameshawahi kuwa kisura wa Nokia na balozi wa Glo deals ambazo zilimpa cash ndefu na pia akijihusisha na biashara zake.

5 Mercy Johnson – Naira Milioni 55

Watanzania wanamfahamu sana muigizaji huyu ambaye amewahi kushirikiana na wasanii wengi wa Bongo Movies akiwemo marehemu Steven Kanumba na Pastor Muyamba.

Mwaka 2008, Mercy Johnson alikuwa ameshaonekana kwenye filamu 15 ambazo zilimpa kiasi cha Naira milioni 11.4.

Mwaka uliofuatia aliingiza Naira milioni 13. Anawekeza kwenye mijengo zaidi na tayari anayo kama sita jijini Lagos.

6 Omotola Jalade Ekeinde – Naira milioni 53

Zilimtoka zaidi ya milioni 10 Wema Sepetu kumleta Omotola Tanzania kwenye uzinduzi wa filamu yake Superstar.

Inadaiwa kuwa mrembo huyu huendesha gari zenye thamani zaidi kuliko msanii mwingine yeyote wa Nigeria. Parking yake ya magari nyumbani inakadiriwa kuwa na ndinga zenye thamani ya Naira milioni 20.

Pamoja na kuigiza, Omotola ni mwanamuziki na ambaye ana albam kama ‘Gba’ na ‘Me, Myself & Eyes’. Inadaiwa kuwa production na promotion ya albam yake ya pili iligharimu kama naira milioni 13 hivi.

7 Patience Ozokwor – Naira milioni 51

Katika sehemu za mwanamke mkali na mkuda kwenye filamu za Nollywood hakuna muigizaji mwingine wa kike anayemfikia mama huyu ambaye hujulikana kwa jina la utani kama Mama G.

8) Monalisa Chinda – Naira milioni 50

9 Uche Jombo – Naira mlioni 49.5

10) CHIOMA CHUKWUKA – Naira milioni 46

Ameshaigiza karibu filamu 70 ambazo zimemuingizia mkwanja mrefu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents